Kampuni ya teksi ‘Uber’ inatarajia kutengeza magari yanayoruka baada ya kukamilika kwa utafiti unaofanywa na kampuni hiyo kuhusu gari hizo.
Muhandisi wa zamani wa shirika la maswala ya angani Nasa, Mark Moore ambaye ni mkurugenzi wa uhandisi wa angani katika kampuni ya Uber ndiyo anayeongoza utafiti huo kuhusu kuanzisha magari yanayoruka.
Moore amesema kuwa mpango wa kutengeza vitu vinavyopaa kielektroniki ni mpango muhimu wa kiteknolojia wa ndege na kuongezea kwamba kitu kinachozuia kuanza kwa mpango huo ni betri zitakazotumika.
Uber tayari inawekeza katika magari ya kujiendesha ikishirikiana na kampuni ya Volvo na Daimler.
Katika mipango yake Uber imesema kuwa katika mahitaji ya angani ,kampuni hiyo ina uwezo wa kuimarisha uchukuzi wa mijini na kuwapatia wateja wake muda wanaopoteza kila siku wanaposafiri.