Kampuni inayotayarisha michezo ya kompyuta ya Razer imezindua laptop mpya yenye skrini tatu kwenye maonyesho ya teknolojia mpya jijini Las Vegas, Marekani.
Kampuni hiyo imesema laptop hiyo ambayo imeundwa kupitia mradi uliopewa jina la Valerie, ndiyo ya kwanza ya aina yake duniani.
Skrini zote tatu zina ukubwa wa wa inchi 17 ( sawa na sentimita 43) na uwezo wake ni pikseli 4,000 (4k), skrini mbili huchomoza kila upande kutoka kwa skrini kubwa ya kati, moja kwa moja. Sifa nyingine ni kuwa, kompyuta hiyo inapozimwa na kufungwa, inapungua upana wa inchi 1.5.
Mmoja wa wachanganuzi wa teknolojia mpya amesifu laptop hiyo na kusema wachezaji wa michezo ya kompyuta siku hizi wamekuwa wakitafuta kompyuta za kisasa zaidi, ghali na zenye uwezo wa kipekee
Razer wamesema inalingana na laptop nyingi zinazotumiwa kwenye michezo ya kompyuta, ambazo kawaida huwa kubwa kidogo kuliko kompyuta zinazotumiwa nyumbani na afisini.