Kesi hiyo ya Nokia imewasilishwa katika mahakama tatu nchini Ujerumani na Texas nchini Marekani.
Madai hayo yanashirikisha matangazo, matumizi ya Interface, programu ,antena, chipu na alama za siri za video.
Juzi kampuni ya Apple ilianzisha mashtaka dhidi ya kampuni ya utafiti ya Acacia Research pamoja na kampuni ya umiliki wa mali ya Conversant Intellectual Property managament ikidai kuwa ilishirikiana na Nokia kuilaghai fedha Apple.
Taarifa ya Nokia inasema kuwa tangu kuweka makubaliano kuhusiana na leseni zinazosimamia teknolojia hizo kutoka kwa Nokia 2011, Apple imekataa maombi yaliofanywa na Nokia kuzipatia leseni baadhi ya tekenolojia zilizovumbuliwa ambazo hutumika na bidhaa nyingi za Apple.
Kati ya mwaka 2009 na 2011,kampuni hizo mbili zilikabiliana mahakamani kuhusu uvumbuzi huo wa kiteknolijia uliotumika katika simu zao.
Wakati huo Nokia ilikuwa inaongoza kama kampuni inayootengeza simu duniani lakini ikawa inakandamizwa na kuimarika kwa iPhone ya Apple.