Kampuni Ya Saruji ya Dangote inatarajia kushiriki ujenzi wa makao makuu ya Serikali Dodoma kwa kusambaza saruji ya kutosha, ya bei nafuu na yenye ubora.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana ameseema kuwa wamefanya mazungumzo na viongozi wa kampuni hiyo ipo tayari kusambaza saruji ya kutosha mkoani hapo.

Rugimbana amesema ujenzi wa miji katika halmashauri zinazozunguka Mansipaa ya Dodoma, saruji inahitajika kwa wingi, hivyo kitendo cha kampuni hiyo kukubali kusambaza kwa wingi kuharakisha ujenzi wa miji hiyo.

Meneja wa Dangote Kanda ya Kati, Mselem Ally alipongeza uongozi wa mkoa kwa kutoa eneo ambalo watajenga kituo cha kusambazia saruji katika Kanda ya Kati, mikoa jirani na katika nchi jirani za DRC, Rwanda na Burundi.

Ally amesema kutokana na kampuni hiyo kuwa magari yake zaidi ya 600, itasambaza yenyewe na hiyo itachangia bei yake kuwa ndogo ukiliganisha na saruji ya kampuni nyingine.

Kwa sasa bei ya saruji aina ya 32.5R imeshuka hadi Sh 10,000 kwa mfuko wa kilo 50, wakati 42.5R imeshuka hadi Sh 10,500 kwa mfuko wa kilo 50 kutoka kiwandani Mtwara hadi popote Dar es Salaam na pia itashuka mkoani Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *