Kampuni ya Bima ya Afya ya AAR, imetoa msaada wa vifaa vya usafi vyenye thamani ya Sh mil 10 kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda lengo likiwa kuunga mkono jitihada za serikali kuhakikisha jiji hilo linakuwa safi.

Meneja Masoko wa AAR, Tabia Massudi amesema vifaa vilivyotolewa ni magudulia ya taka 50, reki 20, mafyekeo 15, mabuti 18, glovu 15, pamoja na matoroli 20.

Meneja huyo amesema msaada huo pia umezingatia mojawapo ya vipaumbele vya serikali iliyopo madarakani ambayo ni utunzaji wa mazingira na uhifadhi wa taka.

Pia meneja huyo amesema huo ni mkakati endelevu wa kusaidia kampeni za uhamasishaji, ushiriki wa jamii na kupunguza tatizo la taka katika Jiji la Dar es Salaam huku akisema anaamini vifaa hivyo vitagawanywa katika maeneo ambayo yameathirika zaidi na uchafu.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa ameishukuru kampuni hiyo na kuendelea kusisitiza wakazi wa Mkoa huo kuendelea na usafi lengo likiwa ni kuliona Jiji linakuwa na muonekano mzuri na safi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *