Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishina Simon Sirro amesema kuwa upepelezi wa sakata la kutekwa kwa Roma na wenzake unaendelea ili kubaini walipo.

 

Kamanda Sirro amesema hayo baada ya kelele za watu kwenye mitandao ya kijamii ndani ya siku tatu, huku wasanii, wanasiasa pamoja na wadau mbalimbali wa muziki kuja juu juu ya suala la kupotea vijana hao katika mazingira ya kutatanisha huku wengine wakihusisha tukio hilo na masuala ya kisiasa yanayoendelea nchini.

 

Aidha Kamanda huyo amesema mpaka sasa wameshaunda timu ya uchunguzi na inaendelea vizuri katika upelelezi huku akiwataka wananchi kuwa na subra kwa kuwa upelelezi ndiyo utasema kila kitu.

 

Kwa upande mwingine amewataka watu waache tabia ya kujifanya wao ndiyo ‘Kamishna Sirro’ na kutaka kuzungumzia habari za upelelezi hivyo amewataka watu kuliamini jeshi la Polisi kwa kuwa hawapendi vitendo hivyo viwepo na viendelee kutokea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *