Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema kuwa ametuma timu ya wapelelezi kwenda jijini Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya kufanya mahojiano na Tundu Lissu.
Toka Lissu kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana mwezi Septemba 7, mwaka huu mjini Dodoma Polisi walikuwa bado haijafanya mahojiano naye.
IGP Sirro amesema wametuma wapelelezi Nairobi baada ya kusikia Lissu amekubali kuhojiwa juu ya tukio hilo na matarajio yao pia ni kumpata dereva na mlinzi wake.
IGP Sirro amesema lengo kubwa la mahojiano ni kujua mazingira ya shambulio yalikuwaje na kwamba ikiwezekana wampate dereva na msaidizi huyo wa Lissu ili kurahisisha upepelezi wa tukio lenyewe.
Tangu kutokea kwa tukio hilo Novemba 7 mwaka huu hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa na jeshi hilo kuhusu tukio hilo.