Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam, Kamishina Lazaro Mambosasa amewapa salamu watu wote wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu Jijini humo.
Kauli hiyo amesema leo jijini Dar es Salaam wakati akiongea na waandishi wa habari kwa maa ya kwanza toka ateuliwe na IGP, Simon Sirro kuwa kamanda mkuu wa kanda maalum ya Dar es Salaam.
Kamanda Mambosasa ametamka kuwa yeye yupo kikazi zaidi na hivyo wahalifu watafute mikoa mingine ya kukimbilia na sio Dar es salaam.
Hata hivyo Mambosasa ameeleza kuwa katika kipindi chake atahakikisha Polisi wake wanafanya kazi kwa uweledi mkubwa ili kuepuka uonevu kwa Wananchi.
Mambosasa amesema kuwa yote hayo yatafanikiwa endapo wananchi watashirikiana na Jeshi la Polisi ili kupafanya Dar es salaam kuwa sehemu ya amani na utulivu.