Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amesema kuwa ili kujiunga na lebo yake ya WCB lazima uwe umetoka katika maisha ya chini kabisa kwenye familia isiyojimudu kiuchumi.
Diamond amesema hawawezi kuchukua watu wanaotokea familia zinazojimudu kiuchumi kwa sababu ni vigumu kwa wao kupambana kwa kuwa kila kitu wanacho nyumbani kwao.
Mwanamuziki huyo amesema kuwa sifa ya kwanza WCB ni mtu aliyetoka katika hali ngumu ya maisha ili hawezi kujituma na kuangalia familia yake aliyoiacha.
Diamond amesema kuwa anaamini watu kutoka mtaani wanakuwa na talent ya kweli, wanakuwa na njaa ya kujituma na nidhamu kwa sababu wanaogopa wasije wakarudi tena katika mtaa na kuendelea maisha ya hapo awali.
Lakini kwa mtoto wa kitajiri wanakuwa hawana nidhamu kwa sababu wanajua kwao kuna hela kwa hiyo hawezi kufanya kazi kwa bidii.
Diamond amesisitiza ni mara kumi wakatumia nafasi walionayo kuwasadia wale walio mtaani kwa sababu wapo wengi na wanahitaji kushikwa mkono ili baadae wazisaidie familia zao.