Mwanamuziki wa hip hop Bongo, Kala Jeremiah amesema kuwa alipokea kwa mshtuko taarifa za makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan baada ya kuhusifia wimbo wake ‘Kijana’.
Makamu wa Rais alimsifia Kala Jeremiah kwa nyimbo yake mpya inayoitwa ‘kijana’ ambayo ina hamasisha vijana kufanya kazi kwa bidii.
Mama Samia alifunguka hayo kwenye kikao cha CCM kilichofanyika Dodoma ambapo alikuwa anawaasa wasanii wa Bongo fleva kuimba nyimbo za kuhamasisha na kufundisha jamii.
Makamu wa Rais amesema kuwa umefika wakati wasanii watunge nyimbo kama ya Kala Jeremiah ‘kijana’ ambayo inawaasa vijana wenzake kufanya kazi kwa bidii na juhudi zote ili tu waweze kujenga taifa.
Baada ya kumwagiwa sifa hizo mbele ya waandishi wa habari wote Kala amefunguka haya ili kuelezea ni jinsi gani alijisikia na anachukulaje heshima hiyo aliyopata kutoka kwa kiongozi mkubwa serikalini;
Kala ni moja kati ya wasanii wachache nchini aliyejipatia umaarufu kwa kuimba nyimbo za siasa na nyimbo ambazo zinagusa matatzo ya kijamii tofauti na wasanii wengine ambao huimba mapenzi na vitu vingine vya tofauti.