Mwigizaji nyota wa Bongo Movie, Kajala Masanja na bintiye Paula Kajala kuja na onyesho la kipindi cha ukweli(Reality Show) kwa jina ‘Mom & Doughter “Like Twins”.
Kajala alitangaza ujio wa kipindi hicho hivi karibuni kupitia ukurasa wake wa Instagram akimtaja Lamata Leah kuwa ndiye atakayekuwa muongozaji wa kipindi hicho.
Vile vile Kajala katika taarifa yake hiyo aliiweka sambamba na picha alizopiga na binti yake huyo iliyowaonesha wakiwa pamoja katika mapozi na mavazi tofauti.
Lamata ambaye ni muongozaji na muandaaji wa filamu nchini kupitia Instagram, alieleza kipindi hicho kitakuwa jukwaa la wafuatiliaji wa wawili hao kuujua ukweli wa maisha yao.