Muigizaji wa Bongo Movie, Kajala Masanja na mpenzi wake Harmonize wameendelea kufurahia mapenzi yao baada ya kurudiana.
Harmonize na Kajala walirudiana mwezi Mei mwaka huu baada ya kutengana katika hali tatanishi tangu mwezi Aprili, mwaka jana.
Miezi mitano iliyopita Harmonize alimtema mlimbwende wa Australia aliyekuwa mpenzi wake aitwaye Briana Jai na kuanza juhudi za kufufua penzi lake na Kajala au Mama Pau.
Harmonize amesema kuwa hisia zake kwa Kajala bado zilikuwa hai na alikuwa hana hisia hata tone kwa Briana.
Kajala mwenye umri wa miaka 39 anakiri kuwa mapenzi yake kwa Harmonize yamezidi maradufu kadiri siku zinavyosonga.
Kajala ambaye kwa sasa siyo mchumba wa Harmonize pia ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa timu ya usimamizi ya Lebo ya Konde Music Worldwide anafunguka siri ya kuongezeka kwa mahaba yake kwa jamaa huyo.
Kajala alianza rasmi kazi yake ndani ya Konde Gang miezi miwili iliyopita baada ya Harmonize kumpa wadhifa huo.