Muigizaji wa Bongo Movie, Kajala Masanja amechaguliwa kuwa meneja wa mwanamuziki Harmonize chini ya Konde Gang na kusimamia kazi zake.
Hayo yote yanakuja baada ya Meneja wa Harmonize wa kike anayeitwa Mjerumani kufuta kila kitu kwenye bio yake kuwa meneja wa Harmonize na kuwa anafanya kazi Konde Gang.
Taarifa hii inakuja baada ya Harmonize na menejiment yake kutangaza kuwa Kajala ambaye ni mpenzi wake na Harmonize kuwa meneja mkuu wa Konde boy.
Harmonize alikuwa na mameneja watatu ambao ni Chopa, Jembe ni Jembe na Mjerumani sasa ameongezeka Kajala kwenye lebo hiyo ya Konde Gang.