Muigizaji wa Bongo Movie, Kajala Masanja amesema kuwa, hakuna kitu kinachomtesa kama upweke wa kummisi mwanawe Paula ambaye yupo masomoni nchini Uturuki.
Kajala mesema kuwa anajitahidi kusahau na kuwa bize na mambo mengine lakini ukweli ni kwamba anammisi mwanae huyo..
Amesema kuwa kutokana na upweke huo yeye anachofanya ni kumuombea ili aweze kumaliza masomo yake salama na arejee nyumbani, waungane tena kama zamani.
“Ni kweli naweza kusema upweke wa kutokuwepo kwa Paula unanikabili, lakini ninachofanya ni kumuombea kwa Mungu siku zote arejee salama na afaulu masomo yake vizuri” Alisema Kajala
Paula kwasasa yupo masomoni nchini Uturuki ambapo amepekekwa huko kwa ajili ya kujiendeleza kimasomo.