Muigizaji wa Bongo Movie, Kajala Masanja amedai kuwa hajashindwa kumlea mtoto wake Paula kama watu wanavyodai.
Kauli hiyo ya Kajala imekuja kufuatia watu kumlaumu muigizaji huyo ameshindwa kumlea mtoto wake kutokana na mtoto huyo kukosa maadili.
Kajala amsema kuwa anatamani awaoneshe watu hao malezi anayompatia binti yake huyo.
Kajala ameongeza kwamba katika jambo linalomuumiza ni watu kutumia jina la binti yake hyo na kujifanya ni yeye na wakati mwingine kuweka vitu vibaya ambavyo vinamfanya mtoto wake achukuliwe tofauti katika jamii.
Pia Kajala ameitaka serikali kushughulikia matatizo yanayotolewa na watumiaji wa mitandao kwa umakini wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na kuweka nguvu ya kutosha.
Paula ambaye ni mtoto wa muigizaji huyo pamoja na Producer P- Funky Majani aliwahi kukutwa na mkasa wa kufananishwa na binti aliyerekodiwa akiwa mtupu na kusambazwa mitandaoni.