Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amemuapisha Jaji Ibrahimu Juma kuwa kaimu Jaji mkuu wa Tanzania.

Profesa Ibrahimu anachukua nafasi ya Jaji Othuman Chande ambaye amestaafu wiki hii baada ya kudumu kwenye nafasi hiyo toka mwaka 2010.

Kaimu Jaji Mkuu Ibrahim Juma akikabidhiana na nyaraka na Rais Magufuli baada ya kula kiapo cha utii.
Kaimu Jaji Mkuu Ibrahim Juma akikabidhiana nyaraka na Rais Magufuli baada ya kula kiapo cha utii jana.

Sherehe za kuapisha kaimu Jaji mkuu zimefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo jaji mkuu mstaafu Othuman Chande.

Baada ya kula kiapo kaimu Jaji mkuu Ibrahim Juma amesema kuwa atahakikisha anafanya kazi kwa uadilifu na kuendeleza aliyefanya mtangulizi wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *