Wasanii wa Bongo Fleva, Jux na Darasa wamemjia juu Harmonize baada ya majina yao kuonekana kwenye orodha ya wasanii wakataotumbuiza kwenye Tamasha la msanii huyo.
Jux na Darassa wamedai wameshangaza na majina yao kuonekana kwenye orodha hiyo ya wasanii watakaotumbuiza huku kukiwa hakuna makubaliano ya kufanya show kwenye tamasha hilo.
Jux ameandika ni vyema uongozi wa Harmonize ungewasiliana na menejimenti yake kabla ya kuweka tangazo hilo mtandaoni, amemtaka kulifuta haraka kwa kuwa yeye Binafsi alimtafuta Konde Boy na kumuelezea hatua alizozipitia kwenye makubaliano kuwa sio sahihi lakini hawakuchukulia Serious Ishu hiyo.
Jux amesema kuwa, “Ni Kweli Harmonize aliwahi Kumtafuta na kumuelezea kuhusu hili Tamasha, na baada ya hapo hawakuongea tena lolote kuhusu malipo na litafanyikaje na ratiba yake ipoje, ila walikubalina vitu vikiwa tayari waambiane kwa ajili ya mikataba, leo aliamka na kukuta tangazo limewekwa tayari kuwa atakuwepo kwenye shoo.
Jux ameongeza kuwa baada ya kuliona Tangazo mtandaoni linasambaa sana likiwa na jina lake, alitafuta Uongozi wa Konde Music lakini hakupewa majibu yanayoridhisha, kisha alimtafuta yeye mwenyewe #Harmonize na kumuelezea na hata baada ya hapo Tangazo hakulitoa na aliliacha liendelee kuwepo kwenye page.
Aidha, Jux ameongeza pia kwamba kuwa kitendo hiko sio sawa kwenye muziki na biashara yake, lakini pia huwa ana mawasiliano binafsi na Harmonize hivyo haelewi Ushikaji Unapitiliza au kumchukulia Poa au Kama Dharau kwa upande wake.
Kwa upande wake, Darassa naye ameshusha malalamiko yake akidai wasanii wanapenda kupeana support lakini ni vyema kama Harmonize angewapa taarifa kabla ya kuwabandika kwenye tangazo.