Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Juma Jux amejitolea kumsomesha mtoto wa Shilole kwa mwaka mmoja ikiwa ni zawadi yake katika sherehe ya harusi ya Shilole na Uchebe.

Jux amesema kwamba anafahamu kuwa mwanamke huyo ni mpiganaji na huwa hachoki kupambana katika kutafuta riziki yake mwenyewe na si tegemezi kwa mtu.

Pia amesema kwamba licha ya kuwa Shilole ni msanii mwenzake lakini pia wao ni marafiki ambao wanashauriana na kutaniana mambo mengi lakini pia anatambua kuwa ana mzigo wa majukumu ya kifamilia.

Jux amesema kuwa “Ni mwanamke ambaye anaamini kwenye kutafuta kipato chake mwenyewe na siyo kupewa. Kwa kulitambua hilo nataka nimpunguzie mzigo kidogo dada yangu, Nitagharamia ada ya mtoto wake mmoja pamoja na mahitaji mengine kwa mwaka mmoja. Naamini nikifanya hivyo nitakuwa nimemsaidia yeye kuweza kusonga mbele katika mapambano mengine” .

Shilole jana alifanya Sherehe ya harusi yake ambayo ilihudhuriwa na mastaa kibao wa filamu na muziki.

Shilole alifunga ndoa na mumewe Uchebe mwanzoni mwa mwezi Disemba na jana ndiyo ilikuwa sherehe ya ndoa hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *