Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Juma Jux amefungukia tetesi za kutoka kimapenzi na mrembo maarufu mitandaoni wa Kenya, Huddah.
Jux anasema kuwa, ukaribu wao siyo wa kimapenzi, bali ni wa kikazi na muda siyo mrefu mashabiki wao wataona kitu kikubwa kutoka kwao.
Madai ya wawili hao kuwa wapenzi yaliibuka mara baada ya kuonekana visiwani Zanzibar wakiwa pamoja.
Jux anasema kuwa, ni kweli walikuwa katika hoteli moja, lakini hakuna lolote lilotokea kati yao, lakini mashabiki wao wataona ni kitu gani hasa walikuwa wanafanya Zanzibar.
“Ni kweli tulikuwa Zanzibar, lakini hatukuwa na ukaribu huo, kuna kazi tulikuwa tunafanya hivyo itakapokuwa tayari watu wataona,” anasema Jux ambaye hivi karibuni alipitia changamoto ya maneno mengi baada ya aliyekuwa mwandani wake, Vanessa Mdee kuanika ujauzito wake kwa mpenzi wake wa sasa, Rotimi.