Klabu ya Juventus imeshindwa kutangaza ubingwa wa Seria A kwa mara sita mfululizo msimu huu baada kufungwa 3-1 dhidi ya Roma jana.

Juve wana alama 85 wakiwa wamesalia na michezo miwili na watatwaa ubingwa wa ligi hiyo iwapo wataichapa Crotone katika mechi ya nyumbani Jumapili ijayo.

Juve jana ndiyo ilikuwa ya kwanza kshinda baada ya Mario Lemina kushinda lakini Daniele de Rossi, Stephan El Shaarawy na Radja Nainggolan waliweka matumaini hai kwa klabu yao ya Roma.

Juve walihitaji alama moja kuchukua taji lao kwa mara ya sita mfululizo na walikuwa katika hali nzuri pale Lamina alipoingiza mpira kwenye neti kutoka kwa krosi safi ya Higuain.

Juventus bado wana uhakika wa kunyakuwa taji hilo mbele ya mashabiki wao katika mechi ya nyumbani watakapokutana na Crotone siku ya Jumapili.

Juve wanaweza kuibuka mabingwa siku ya Jumamosi, hata hivyo, iwapo Roma itapoteza kwa Chievo na kuifanya Napoli kuwa katika nafasi ya tatu iwapo hawataichapa Fiorentina nyumbani.

Juventus watabaini iwapo bado watanyakuwa ubingwa wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya katika fainali dhidi ya Real Madrid, mechi inayotarajiwa kuchezwa tarehe 3 mwezi Juni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *