Mwanamuziki nyota wa Marekani, Justin Bieber amehairisha ziara yake ya kimuziki kwa ajili ya kumrudia mungu.
Taarifa ya kuhairishwa ziara hiyo ni hatua yake ya kutaka kujikita zaidi kwenye masuala ya kiimani ikiwezekana kuanzisha kanisa lake.
“Ninalazimika kuamini kuwa sababu halisi ya kuachana na ziara yake ni kutaka kuirudia zaidi imani yake na anaweza hata akawa na mpango wa kuanzisha kanisa lake mwenyewe,”.
Bieber ambayee alilelewa katika familia iliyokuwa ikishikilia imani ya dini ya kilokole ambapo mama yake mzazi alikuwa muumini wa dhehebu moja la kilokole (born again), amekuwa akieleza mara kadhaa kuwa anasikia wito wa kumrudia Yesu.
Hata hivyo, kuna taarifa kuwa huenda Bieber ameamua kuahirisha ziara hiyo ili aweze kupumzisha koo lake kutokana na matatizo ya kiafya yanayowapata wasanii wengi kwa kufanya matamasha mengi bila kupumzika.
Mwimbaji John Mayer ambaye ni mtu wa karibu wa Bieber amesema kuwa endapo angeendelea na ziara hiyo huenda angejiumiza kama walivyofanya wasanii wengi wakubwa ambao amedai wamepotea kutokana na tatizo hilo