Jumla ya watu 116 raia wa Nigeria wameuawa nchini Afrika Kusini kwa njia ya kiholela kwa muda wa miaka miwili iliyopita, kwa mjibu wa gazeti la Daily Trust lililomnukuu afisa mmoja wa serikali.
Abike Dabiri-Erewa, afisa wa cheo cha juu kwenye ofisi ya masuala ya nchi za kigeni, aliyasema hayo wakati alikutana na balozi wa Afrika nchini Nigeria Lulu Louis mjini Abuja.
Anasema kuwa saba kati ya mauaji ya watu 10 yamefanywa na polisi.
Hata hivyo gazeti hilo halijaeleza ni kipindi gani watu hao 116 waliuawa, lakini limezungumzia kuchukuliwa kuwa wahalifu, raia wa Nigeria walio nchini Afrika Kusini.
Mauaji ya hivi majuzi ya raia wa Nigeria nchini Afrika Kusini yalitokea mwezi Disemba mwaka uliopita, wakati polisi mjini Cape Town walimuua kwa kumkosesha pumzi Victor Nnadi.