Shirikisho la soka nchini Hispania “RFEF” limemtangaza rasmi, Julen Lopetegui kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa akichukua nafasi ya Vicente del Bosque aliyebwaga manyanga baada ya kufungwa na Italia na kutolewa kwenye mashindano ya Euro nchini Ufaransa.

Del Bosque ameifundisha timu  ya Hispania miaka minane na kuweka historia na timu hiyo ambapo ameiwezesha kuchukua mataji mawili ya kombe la dunia 2010 pamoja na kombe la mataifa ya Ulaya mwaka 2012.

Lopetegui alianza kazi ya ukocha akiwa kama kocha msaidizi kwenye timu ya taifa ya Hispania chini ya miaka 17 kabla ya kujiunga na Rayo Vallecano na Real Madrid Castilla na mwaka  2010 akaichukua timu ya Hispania chini ya umri wa miaka 19 na kuiwezesha kushinda taji la mataifa ya Ulaya mwaka 2012.

Baada ya hapo kocha huyo alijiunga na FC Porto ya nchini Ureno na kuiwezesha kufika robo fainali ya michuano ya Ulaya “UEFA” kwenye msimu wake wa kwanza.

Ilipofika Januari mwaka huu, Lopetegui alifukuzwa na Porto baada ya kushinda nafasi ya tatu kwenye ligi ya Ureno huku ikitolewa hatua ya makundi kwenye michuano ya Ulaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *