Jukwaa la Wahariri nchini ‘TEF’ limepinga uamuzi wa Serikali kupitia Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo baada ya kuvifungia vyombo vya habari viwili vya Radio 5 ya Arusha na Magic FM ya jijini Dar es Salaam kwa muda usiojulikana.

Katibu wa Jukwaa hilo, Nevile Meena amepinga uamuzi huo huku akieleza kuwa Waziri Nape hakueleza makosa ya kiundani juu ya vyombo hivyo mpaka kufikia kufungiwa kwa muda usiojulikana na kwamba hakutoa historia ya mwenendo wa awali wa vyombo hivyo.

Pia amesema ni muda mfupi waziri huyo ambaye ndiyo mlezi wa vyombo vya habari, Nape Nnauye kujitokeza mara nne na kufungia vyombo vya habari mbali mbali yakiwemo magazeti na majarida.

Aliongeza kwa kusema kwamba TEF inaona uamuzi wa Waziri Nape hauna nia njema na kifungu alichotumia kuvifungia vituo hivyo havimlazimishi kufanya hivyo.

Waziri Nape juzi alitangaza kuvifungia vituo viwili vya radio nchini ambavyo ni Radio 5 ya Arsha na Magic FM kwa kosa la kukiuka kanuni na sheria na kanuni za utangazaji kwa kurusha vipindi vyenye maudhui ya uchochezi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *