Aliyekuwa makamu wa rais wa Sudan Kusini, Dkt Riek Machar ameondoka nchini humo wiki chache baada ya mapigano makali kuzuka kati ya vikosi vyake na wanajeshi watiifu kwa Rais Salva Kiir mjini Juba.

Msemaji wake James Gatdet Diak amesema kiongozi huyo amefanikiwa kuhamia taifa jirani, ambalo hakulitaja jina.

South Sudan's rebel leader Riek Machar speaks during an interview with Reuters in his office in Addis Ababa

Rais Kiir alimfuta kazi Dkt Machar mwezi uliopita na nafasi yake kuchukuliwa na Bw Taban Deng Gai.

Dkt Machar hapo awali amesema hatarejea Juba hadi kuwepo na kikosi cha wanajeshi wasioegemea upande wowote cha kumlinda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *