Wachekeshaji maarufu nchini, Joti na Mpoki watashiriki katika mechi ya kirafiki kati ya timu ya Mbwana Samatta anayekipiga KRC Genk ya Ubelgiji na timu ya mwanamuziki nyota nchini Ali Kiba.

 

Mechi hiyo kusaidia elimu nchini, waigizaji maarufu nchini, Lucas Mhavile ‘Joti’ na Sylvestre Mjuni ‘Mpoki’, nao wameingia.

Joti na Mpoki sasa watakuwa wasemaji wa mechi hiyo itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa Juni 9 jijini Taifa jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa mechi hiyo, Hussein Hembe, amesema kuwa licha ya Joti na Mpoki kuungana na Samatta pamoja na Kiba katika mechi hiyo pia wamepewa majukumu ya kufanya.

Alisema Joti amepewa jukumu la kuwa msemaji wa timu itakayoundwa na Samatta wakati Mpoki msemaji wa timu itakayoundwa Kiba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *