Muigizaji wa maigizo na mchekeshaji maarufu, Joti anatarajia kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu hivi karibuni.
Msanii huyo hivi karibuni ameonekana katika mitandao ya kijamii yeye na mpenzi wake huyo katika picha za pamoja ikiwa ni pre-wedding photshop.
Joti ambae alianza maigizo ya uchekeshaji miaka mingi nyuma na baadae kuingia katika kundi la Orijono Komedi anategemea kufunga ndoa na sherehe kufanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar Es Salam.
Akiandika katika moja ya post zake katika ukurasa wake wa instahram Joti aLiweka picha aliokuwa pamoja na mkewe huyo na kuandika “alilopanga mungu..” hata hivyo baadhi ya picha zilimuonyesha msanii huyo akiwa na rafiki zake wa karibu katika send-off party ya mke wake.
Baadhi ya mashabiki wameonekana kufurahishwa na jambo hilo na kumpongeza msanii huyo, huku wengine wakidhania ni utani kama ilivyozoeleka hapa awali ambapo Joti amekuwa akiweka picha za harusi na wadada tofauti kumbe alikuwa katika moja ya kazi zake za matangazo.
Baadhi ya wasanii wenzie walimpongeza msanii huyo na mmoja wapo alikuwa ni mchekeshaji mwenzie Masanja Mkandamizaji.