Mchekeshaji maarufu nchini, Lucas Mhavile ‘Joti’ amesema kuwa sasa ameamua kuja kivingine kwenye nyanja ya uchekeshaji kwa kutumia Youtube Tv kuwaletea mashabuki wake burudani.
Joti ambaye ni memba wa kundi la Olijino Komedi amesema kuwa ameamua kutumia Yotube Tv kuwasilisha ujumbe wake wa vichekesho akiamini sasa hivi dunia iko kwenye kiganja kutokana na teknolojia kupanuka.
Mchekeshaji huyo amesema kuwa Tv hiyo imelenga nyanja zote na imeangalia sana watoto kwa sababu kitu akikipenda mtoto basi na mzazi atakipenda, pia kutoa elimu kwa watoto katika uchekeshaji atatoa elimu kwa watoto na mambo mengine mengi makubwa ya watoto yanakuja.
Joti amesema watoto ni watu ambao wanaupendo wa kweli hawana unafiki na ndio vipaji ambavyo vinatakiwa kuendeleza kwa kuliona hilo nikaona hamna haja ya kuacha vipaji vyenye upendo wa kweli vipotee ni bora niwe navyo bega kwa bega.
Mkali huyo amefafanua kuwa Chaneli yake itahusika na shughuli zake pekee mtu asitegemee kuona taarifa za habari na mambo mengine kama chanel za watu wengine.
Pia Joti amesema kuna wachekeshaji wengi chipukizi wanafanya vizuri ila hawataki ushauri, wala hawana mtu waliyempenda ili kuingia katika hiyo kazi hili nitatizo na mtu kuwa staa lazima uwe na historia huwezi kukurupuka na kuwa staa.