Mwanamitindo maarufu Bongo, Jokate Mwegelo amefunguka na kudai kuwa anategemea kutumia nafasi aliyonayo katika chama chake na umaarufu katika jamii katika kuhakikisha anasimamia haki za wanawake na watoto.
Jokate ni moja tu kati ya mastaa walioamua kugeukia siasa, ambapo kupitia chama cha mapinduzi anashikili nyadhfa fulani. Jokate amesema kwa kupitia nafasi aliyonayo atahakikisha kuwa anapambana awezavyo kuhakikisha anapambania haki za wanawake pamoja na watoto kwa ujumla.
Kwenye mahojiano aliyoyafanya na kipindi cha Star Mix, Jokate alidai kuwa kuna umuhimu sana kila mmoja mwenye nafasi kwenye jamii atambue umuhimu wa mwanamke kwani wao ndio wenye nafasi kubwa kwenye jamii na hivyo wakazane katika kuhakikisha wanawapa elimu.
Unajua watu wengi wanajisahau kuhusu mwanamke na mtoto lakini kwa upande wangu nawaona wana nafasi kubwa sana ya hasa mwanamke akipewa elimu bora na kupewa nafasi nyingi za kuongoza huku watoto wakipewa haki inayostahili”.
Jokate ambaye anamiliki kampuni yake ya kidoti inayofanya vizuri amezidi kung’aa na mafanikio take kuonekana hadi nje ya nchi hasa pale ambapo mapema mwaka huh alichaguliwa kama mmoja Kati ya vijana 100 mwenye ushawishi nchini Afrika lakini pia ameamua kugeukia siasa na siku za hivi karibuni ameonekana akijikita zaidi katika kuisaidia jamii katika mambo mbali mbali yenye umuhimu na yenye kujenga taifa letu.