Muigizaji wa Bongo Movie, Johari amefunguka na kusema kuwa amejitia nuksi ya ndoa baada ya kuigiza anaolewa katika movie tatu mfululizo.

Johari amesema kuwa kipindi kile walichokuwa wakiigiza wamevaa mashela ndipo walijitia nuksi na mashela hayo yakaondoka na ndoa zao mpaka leo hii, maana yeye aliigiza zaidi ya mara tatu kuwa ameolewa na kuvaa shela.

Johari anasema kuwa, amejifunza kitu kikubwa sana katika kuigiza unaolewa na wakati hujaolewa ni kitu ambacho kitakupa nuksi tu maana kwenye ulimwengu wa roho tayari umeshafunga ndoa feki ambayo inazuia ndoa za kweli kuja.

“Mashela ndiyo yameharibu kila kitu na hata ndoto za kuolewa kweli kwa sababu inaonekana kiroho tumeshaolewa, sasa kama mimi jamani nimevaa mashela mara tatu hiyo unaichukuliaje sasa kuna ndoa tena hapo.

Kwa hiyo nimeseme tu kwamba mashela yameondoka na ndoa zetu,” anasema Johari ambaye amekuwa akitamani kuolewa kwa muda mrefu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *