Muigizaji wa Bongo Movie, Johari amefunguka na kudai kifo cha marehemu Steven Kanumba kimewaathiri kwa kiasi kikubwa katika utendaji kazi wao kwa maana walikuwa wanatoa kazi kwa kushindana baina yao.

Johari amebainisha hayo wakati alipokuwa anajibu swali kutoka kwa miongoni mwa shabiki zake aliyetaka kufahamu kama ni kweli marehemu Steven Kanumba amekufa na bongo movie yake ?, kwa madai kwa sasa hakuna kazi nzuri zinazofanywa kama kipindi alipokuwa hai Kanumba.

“Kuna vitu vingine vinakatisha tamaa ila kwa upande wangu siwezi kuamini hilo kwasababu watanzania tuna kawaida moja ya kumsifia mtu akiwa amefariki kushinda akiwa hai. Kanumba alikuwa na mashabiki zake, nasi pia tuna mashabiki zetu ‘so’ siwezi kuamini kwamba mashabiki zetu wote wamehama kutokana na mtu moja kufariki. Hiki mimi siwezi kuamini kwamba kifo cha Kanumba kimeuwa bongo movie”,.

Pamoja na hayo, Johari ameendelea kwa kusema “kuondoka kwa Kanumba siwezi kusema kimeshusha au kupandisha. Binafsi ninachokiona alipofariki Kanumba kuwa kuna baadhi ya watu wameathirika kwa kiasi fulani au niseme sisi hapa ndio tumeaumizwa na kifo chake kwasababu tulikuwa tunapenda ushindani wa kazi na kampuni yake”.

Kwa upande mwingine, Johari ameitaka jamii kuacha kutoa kauli zenye lengo la kuwavunja moyo kwa kuwa bongo movie ipo hai na wasanii wapo wengi waliokuwa wazuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *