Muigizaji maarufu wa Bongo Movies, Blandina Chagula (Johari) amefunguka sababu za yeye kutokuwa na mume mpaka sasa huku akianika kwamba yupo tayari kuolewa na mwanaume wa aina yoyote.

Katika mahojiano aliyofanya hivi karibuni na moja ya chombo cha habari, Johari amesema; “Mimi ni mkubwa kiumri kwa kweli Watanzania mjue kua mimi ni mkubwa.

“Wanaume wapo wengi wanaotaka kunioa ila wote unakuta washaoa wanataka niwe mke wa pili, mimi kwa kweli siwezi ila kwa sasa nipo tayari kuolewa na mwanaume yoyote.

Pia amesema kuwa sitaki kuchagua sana ila cha muhimu anisaidie na kuni-support katika kila jambo ninalofanya,” amesema Johari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *