Muigizaji wa Bongo Movie, Blandina Chagula ‘Johari’ amefunguka kwa kusema kuwa anatarajia kugombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.
Johari amesema kuwa nia yake sasa ni kuwa mbunge ili aweze kutumikia wananchi kwa karibu kutokana na mapenzi yake kwa wananchi wanaomshabikia.
Pia amesema kuwa ana mpango wa kugombea nafasi hiyo ya uwakilishi mwaka 2020 kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) kwani ndiyo chama chake anachokisapoti toka akiwa mdogo.
Muigizaji huyo aliyejizolea umaarufu miaka ya nyuma ameongeza kwa kusema kuwa hapendi kuchanganya siasa na kazi yake ya uigizaji kwa sababu mashabiki ni wa kada mbalimbali za kisiasa.
Johari ni miongoni mwa waigizaji wa Bongo Movie waliozunguka nchi nzima kukinadi chama cha Mapinduzi wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015.