Wakali wa Hip Hop Bongo, Joh Makini na Dogo Janja leo wanatarajiwa kutoa burudani katika mbio za Kilimanjaro Marathon 2017 mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli, aliwataka wakazi mkoani hapa kujitokeza kwa wingi katika mbio hizo ambazo ni kubwa Tanzania.

“Wasanii hawa wanakubalika Moshi, tuna uhakika mashabiki watajitokeza kwa wingi kuangalia mbio na kupata burudani,” alisema Pamela.

Joh Makini amesema amejiandaa vizuri kukonga nyoyo za mashabiki wake na kuwataka wakazi wa Moshi kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani iliyoandaliwa.

Kwa upande wa Dogo Janja amesema anafarijika kupata nafasi hiyo, kwani mkoa huo ni miongoni mwa mikoa yenye mwamko mkubwa wa mashabiki.

Usajili mjini Moshi ulianza kufanyika siku mbili nyuma, huku wakazi mbalimbali wakiwa wamejitokeza kujiandikisha kushiriki mbio hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *