Mwanamuziki mkongwe wa kike wa Bongo fleva, Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’ amemjia juu na kumtolea povu zito shabiki wake aliyemuombea kwa Mungu azae mtoto.

Lady Jay Dee amekaa kwenye sanaa ya muziki kwa kipindi kirefu sana labda kuliko msanii yoyote wa kike lakini moja kati ya vitu mashabiki wake hupenda kujua kuhusu yeye ni maisha yake binafsi.

Kwasasa Jay Dee amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki kutoka Nigeria anayejulikana kama Spicy Music.

Moja kati ya vitu ambavyo huongelewa sana kuhusu Lady Jay Dee na maisha yake binafsi ni suala la kuzaa mtoto ambapo kumekuwa na tetesi nyingi kuwa hana uwezo wa kuzaa huku tetesi hizi zikizaliwa kutokana na kukaa kwenye ndoa kwa miaka kumi na zaidi bila kupata mtoto na umri wake kusemekana kuwa umeenda Ingawa mwenyewe hajawahi kuliongelea suala hilo hadharani.

Siku chache zilizopita moja wa shabiki wa Lady Jay Dee aliandika kwenye ukurasa wa Lady Jay Dee kuwa anamuombea azae mtoto na anampensa sana maneno yaliyoelekea kumkera Jay Dee.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *