Kamanda mkuu wa jeshi la Zimbabwe, Jenerali Constantino Chiwenga ameonya kuingilia kati iwapo pande pinzani zitaendelea kuzozana ndani ya chama tawala cha Zanu-PF.
Katika taarifa isio ya kawaida , Jenerali Constantino Chiwenga ametaka kusitishwa kwa vita dhidi ya wanachama waliopigania uhuru wa taifa hilo.
Matamshi yake yanajiri baada ya rais Robert Mugabe kumfuta kazi makamu wake wa rais aliyetarajiwa kumrithi Emmerson Mnangagwa.
Kufutwa kwake kunampatia bi Grace Mugabe fursa kumrithi kiongozi huyu mwenye umri wa miaka 93.
Akizungumza katika makao makuu ya jeshi , jenerali Chiwenga alisema: Mgogoro unaoendelea unaowalenga wanachama wa chama hicho waliopiganai uhuru ni lazima ukome.