Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha linamshilkilia mmiliki wa shule ya Lucky Vicent ambayo wanafunzi wake walipata ajali kutokana na kuruhusu gari kubeba zaidi ya watu 30.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha ( RPC ), Charles Mkumbo amesema kuwa wanamshikilia mmiliki wa basi dogo aina ya Coaster ambayo ilipata ajali na kusababisha vifo kwa wanafunzi, walimu na dereva siku ya Jumamosi huko Karatu, Arusha.

Pia Kamanda Mkubo amedai kuwa wanamshikilia mmiliki wa shule hiyo kwa kuruhusu gari yake hiyo kubeba abiria wengi zaidi kuliko uwezo wa gari

Kamanda huyo amesema kuwa “Siku ya tukio walikuwepo abiria 38 kwenye gari katika uchunguzi baada ya kubaini hilo tumeshachukua hatua kwa mtu aliyewezesha gari hilo kupakia hao watu, tumeshamkamata mmiliki wa gari ambaye ndiye mwenye shule hii, sasa hivi tunaendelea na uchunguzi na utakapokamilika atafikishwa mahakamani.

Kwa mujibu wa kamanda huyo amesema gari hiyo ilikuwa na kibali cha kubeba watu 30 lakini gari hiyo siku ya ajali ilikuwa na watu zaidi ya 30.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *