Jeshi la Polisi Zanzibar limesema kuwa halina taarifa za kuonekana kwa mashekhe watatu wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, ambao waliripotiwa kutoonekana tangu Januari 9, mwaka huu.
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Nassir Ali, alisema jeshi hilo lilifanya kazi ya kuwatafuta mashekhe hao, lakini halikufanikiwa kuwaona.
Kamanda huyo ameiasa jamii kuacha kuchanganya mambo ya kihalifu na kisiasa kwa kuwa halileti taswira nzuri kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Ameongeza kwamba awali jeshi hilo lilipokea taarifa rasmi kutoka kwa familia na ndugu wa mashekhe hao, kuwa hawaonekani na wamepotea katika mazingira ya kutatanisha huku likihusishwa jeshi hilo kuwa ndio lililo wachukua.