Mwanamuziki wa RnB nchini Marekani, Chris Brown ameandaliwa kikao cha nidhamu na Jeshi la Polisi mjini Los Angeles baada ya kupokea malalamiko kila wakati kutoka kwa majirani kuhusu kelele na fujo nyumbani kwake.
Kikao hicho kitahudhuriwa na polisi, washauri na majirani wawili wa Chris Brown na sababu ya kikao hichi ni kubadilisha tabia ya Chris Brown.
Fujo hizo ni pamoja na kelele, matumizi ya dawa za kulevya, kupigana, uendesha hovyo wa magari na piki piki.
Chris kuhudhuria kikao hichi sio lazima ila ni ombi kutoka kwa polisi wanaofahami tabia zake.
Chris Brown anajianda kwenda tour ya “Party Tour” na wasanii kama Fabolous, 50 Cent, French Montana, O.T. Genasis, Kap G.