Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewataka wananchi wanoishi maeneo ya mabondeni kuhama wenyewe kwa hiari kabla jeshi hilo alijachukua hatua za kisheria.
Kamishna wa Kanda hiyo, Kamanda Simon Sirro amesema kuwa wananchi waishio mabondeni wanatakiwa kuhama maeneo hayo kutokana na kuatarisha maisha yao ambapo juzi walikubwa na mafuriko kutokana na mvua iliyonyesha Dar es Salaam.
Pia Kamanda Sirro amesema kuwa Jeshi hilo limeokoa mwili wa mtoto wa kike aliyefahamika kwa jina la Imelda Ngonyani (13) aliyekufa maji wakati akijaribu kuvuka mto Msimbazi.
Sirro amesema marehemu huyo kabla ya kufa maji alikuwa pamoja na wenzake watano walionusurika kifo wakielekea shule ya Msingi ya Mongo la Ndege.
Kamanda Sirro ametoa wito kwa wananchi kuwa makini katika kipindi hiki cha mvua za masika zinazoendelea kunyesha, na kuwataka wananchi wanaoishi karibu na mto msimbazi kuondoka kwa hiari ili kujiepusha na athari za mafuriko.
Katika hatua nyingine, Kamanda Sirro amesema Jeshi la Polisi mnamo Machi 12, 2017 maeneo ya Zimbwini kata ya Vijibweni Manispaa ya Kigamboni lilifanikiwa kukamata watuhumiwa wawili wenye umri kati ya 25 hadi 30 wakiwa na bastola moja aina ya Bereta yenye risasi sita ndani ya magazini.