Jengo la makao makuu ya Klabu ya Yanga lililoko maeneo ya Jangwani Kariakoo jijini Dar es Salaam, liko hatarini kupigwa mnada kutokana na deni la Sh. milioni 300 ambalo klabu hiyo inadaiwa.

Taarifa zilizopatikana jana jijini zinaeleza kuwa Kampuni ya Udalali ya Msolopa ndiyo imepewa mamlaka ya kusimamia mnada huo.

Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amethibitisha kuwapo kwa deni hilo na kueleza kuwa uongozi umeanza utaratibu wa kulifanyia kazi suala hilo.

Mkwasa ambaye ni kocha na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo amesema kuwa ni kweli kesi iko katika Mahakama ya Ardhi na tumeshaanza kuifanyia kazi.

Mkwasa amesema kuwa deni hilo limetokana na malimbikizo ya ada ya jengo la kiwanja kinachomilikiwa na klabu hiyo, lakini wanaamini watalilipa kabla ya mchakato huo wa kunadi jengo hilo la makao makuu haujafanyika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *