Mkuu wa jeshi la polisi la Uganda, Jenerali Kale Kayihura anatarajiwa kufika kizimbani leo kujibu mashtaka ya kuwatesa na kuwanyanyasa wafuasi wa upinzani.

Mashataka haya yana uhusiano na kile kinachoitwa unyama wa polisi kufuatia askari polisi kuwatandika wafuasi wa Dkt Kiiza Besigye waliokuwa wakiandamana katika barabara za mjini Kampala hadi makao makuu ya chama cha upinzani cha FDC.

Hatua ya mkuu wa polisi huyo kuitwa mahakamani inafuata juhudi za mawakili wa kampuni ya uwakili ya Namugali na Walyemera kupeleka kesi mahakamani kwa niaba ya wateja wao kadha.

Wamemshtaki kinara wa polisi na pia maafisa wengine saba wa jeshi la polisi kwa ujumla kwa kuwanyanyasa wananchi.

Hata hivyo kuna shaka kuwa huenda Kayihura asifike mahakamani kutokana na matukio kadhaa.

Naibu msemaji wa polisi Namaye amenukuliwa na vyombo vya habari nchini akisema kuwa Jenerali Kayihura hatafika mahakamani kwa sababu hajapata waraka wa kumuita mahakamani.

Lakini wakili Daniel Walyemera Masumba anaeongoza kesi hiyo amekanusha hayo.

Mawakili wanasisitiza kuwa wanataka mkuu wa polisi ajitokeze mwenyewe na wala sio mjumbe wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *