Rais wa Urusi, Vladimir Putin amesema kuwa katika maisha yake hatumii simu ya smart phone wala internet.

Pamoja na kwamba watu wengi nchini mwake, wakiwemo wanafunzi, huchakarika ili kupata aina hizo za simu, Putin amefichua kwamba analitawala taifa hilo la watu milioni 144 bila kutumia smartphone.

Akiwa amekiri pia kwamba hapendi mambo ya technolojia mpya, amesema kamwe huwa hatumii Internet na kama ikilazimika, huwatumia wasaidizi wake kumtafutia kitu anachokitaka.

Amesema pia kwamba hapendi kujiunga katika mitandao ya kijamii, kinyume na mwenzake wa Marekani, Rais Donald Trump, anayetumia mtandao wa Twitter kama silaha yake binafsi ya kisiasa.

Mwaka jana alipokutana na watoto wa shule, Putin aliulizwa iwapo huwa anatazama mtandao wa Instagram au mitandao mingine ya kijamii wakati wake wa mapumziko.

Kauli hizo za Putin zimekuja wakati kuna ripoti kwamba wadukuaji wa mitandao wa Russia wanajaribu kuhujumu chaguzi katika nchi za kidemokrasia za Magharibi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *