Muigizaji wa Bongo Movie, Jacob Stephen ‘JB amesema kuwa hawakufanya maandamano ya kuzuia movie za nje kuuzwa nchini bali waliandamana kuzitaka zilipiwe kodi au serikali itoe msamaha kwenye filamu za ndani.

JB amezungumza hayo wakati wa uzinduzi wa filamu ya Tunu na kudai kuwa watu wengi wamehusisha maandamano yao na siasa kitu ambacho hakina ukweli.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa tasnia ya filamu kwa sasa inahitaji watu watakaowasaidia kumaliza kilio chao.

JB amesema kuwa wasanii wenzao wanaowakejeli kwa kuandamana wengi wao hawategemei movie kuwaingizia kipato na ndio maana wanaongea maneno ya ajabu huko nje.

“Msanii yoyote ambaye filamu ndiyo chakula chake hawezi kuwa nje ya hili kwa sababu hataweza kuishi. Mimi niseme tu siwezi kuishi bila filamu ndiyo maana tunapiga kelele”.

Baadhi ya waigizaji wa Bongo Movie waliodharau maandamano hayo ni muigizaji Wema Sepetu pamoja na Steve Nyerere.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *