Rais wa Marekani, Donald Trump amemjibu Jay-Z baada ya mwanamuziki huyo wa muziki wa Rap kumuita “mdudu hatari” kutokana na kuwachukukia watu weusi.
Katika ujumbe kwenye Twitter Bw Trump alisema kuwa “kiwango cha Wamarekani wasio na ajira kimeripotiwa kuwa cha chini kabisa kuwahi kurekodiwa!” kwa sababu ya sera zake.
WaMarekani wenye asili ya Afrika wasio na ajira ni asilimia 6.8%, kiwango ambacho ni cha chini kuwahi zaidi kurekodiwa.
Lakini wakosoaji wanasema kuwa kiwango cha ukuaji wa uchumi kilianza kuimarika wakati wa rais Obama na kwamba ukosefu wa ajira miongoni mwa watu weusi umesalia kuwa wa kiwango cha juu miongoni mwao kuliko miongoni mwa wazungu.
Aidha amesema kuwa kuchaguliwa kwa Bw Trump kulitokana na kushindwa kutatuliwa kikamilifu kwa masuala kadhaa.
Jay-Z alimuunga mkono Barack Obama wakati wa uongozi wake, na alimsifia Bi Hillary Clinton katika uchaguzi wa mwaka 2016 ambapo Bwana Trump alishinda