Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Jay Meloyi amefunguka na kusema kuwa yeye ni mmoja wa watu waliotawaliwa na mapenzi mpaka kupelekea kuandika nyimbo za mapenzi.
Ukiachilia mbali nafasi ya mziki kwenye maisha yake, nafasi nyingine iliyopo kwenye moyo wa msanii Jay Melody ni suala zima la mapenzi.
Mwanamuziki huyo amefunguka kuwa mapenzi yanachukua nafasi kubwa sana kwake na hajawahi kufikiria yanaweza kumbadilisha.
Kwa ufupi tu Jay Melody akiyaelezea mapenzi ameandika kwamba “Binafsi mapenzi yamechukua nafasi kubwa sana kwangu, sikuwahi kufikiria kama nitaweza kubadilika namna hii na yote hayo ni mapenzi”.