Staa wa muziki Jay Melody ameweka wazi juu maisha yake ya sasa ya muziki bila uwepo wa muanzilishi wa THT, Ruge Mutahaba ambaye ndiyo alimtoa kimuziki.

Msanii huyo ameeleza kuwa kuondoka kwa Ruge Mutahaba hakujapunguza kitu bali kumeongeza chachu ya kufanya kazi

Alisema kuwa “Kwangu mimi haijabadirisha kitu bali imeongeza hasira katika kuendelea kupambana kwa sababu mwisho wa siku ukiendelea kufeli utakuwa wewe ndio umefeli, kwa nini mtu mmoja kaondoka wewe ndio unafeli inaonekana umekuwa mjinga.

Pia alisema baba alitupa knowledge ya kutosha nimekaa naye karibu nimeongea ananiambia Jay nataka wewe ndio unaofuata nataka uwe na ukubwa ambao mimi nautaka,’ameeleza Jay

Akaongeza ‘Kuondoka mtu mmoja haimaanishi ndio unafeli kama kuondoka kila mtu ataondoka, cha msingi ni kuhakikisha kuwa unafanya kile ambacho alikufundisha.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *