Muigizaji wa Bongo Movie, Jacquline Wolper amekanusha taarifa zilizoenea katika mitandao ya kijamii kuwa ameachana na mpenzi wake anayefahamika kwa jina la Brown.

Wolper amesema ingawa kuna vitendo vinavyoashiria kuachana kwa wawili hao ikiwemo kufutwa kwa baadhi ya picha na kutompost mara kwa mara kama siku za nyuma, ni kutokana na baadhi ya mikataba ya kazi aliyoingia.

Ameongeza kwa kusema kuwa “Watanzania wamezoea sana Instagram, usipompost bwana wako basi mmeachana, hawajui hata kama watu mumepata deal, mmeingia mikataba, hautakiwi kuweka mapicha ya mapenzi, mpaka wanataka utoe siri sasa, kuna issue siwezi kuiongelea, hivyo hakuna kitu kama hicho kikiwepo nitaongea”.

Wolper amekutwa na tetesi za kuachana na Brown  baada ya kuonekana akishikana mkono kusalimiana na aliyekuwa mpenzi wake kwenye sherehe ambayo wawili hao walihudhuria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *