Muigizaji wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper amefunguka na kusema kuwa hana matatizo na lebo ya WCB licha ya kuachana na mwanamuziki wa lebo hiyo, Harmonize.

Wolper amesema hayo baada ya kuwepo taarifa mtaani kuwa muigizaji huyo kwasasa si shabiki tena wa WCB na ameacha kusapoti kazi za wanamuziki walio chini ya lebo hiyo inayomilikiwa na Diamond Platnumz.

Wiki iliyopita moja ya mtandao uliripoti kuwa muigizaji huyo kaeleza kuwa yeye si shabiki wa WCB bali Diamond.

Wolper amesema hilo halina ukweli wowote na kueleza kuwa watu wanaoelewa ukaribu wake na WCB hawawezi kutilia maanani hilo.

Wolper aliwahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na muimbaji kutoka lebo hiyo Harmonize ambao kwasasa wameachana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *