Dansa wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz , Mose Iyobo amemfananisha mpenzi wake Ruby na msani wa Marekani Rihana.
Hiyo inajiri baada ya siku kadhaa tu kupita tangu waingie kwenye mahusiano ambayo yanatafsiriwa kama ni kisasi kwa mahusiano yao yaliyopita.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Iyobo amemjaza sifa kibao Ruby huku akimkumbusha kuwa asiende kwa mganga; “Badgalriri shetani aliniwekea vikwazo vingi ila now kashindwa, pray yourself usiende kwa mganga tunguli huisha nguvu,” ameandika Mose Iyobo.
Ikumbukwe kuwa Iyobo aliwahi kuwa kwenye mahusiano na mzazi mwenza Aunty Ezekiel ambaye hivi sasa yupo na msanii wa Bongo Fleva, Kusah ambaye ni Baba wa mtoto wa pili wa Aunty lakini pia aliwahi kuzama kwenye penzi nzito kwa mzazi mwenza Ruby.